A+ R A-

Myrtis

E-mail Εκτύπωση PDF

Myrtis has been named “friend of the United Nations”
Her message to the world leaders


Myrtis died of typhoid fever during the plague which hit Athens in the middle of the 5th Century BC. Typhoid fever is even today -2.500 years after- the cause of death for 500.000 to 700.000 people every year. Moreover, each year nearly nine million children under five are losing their lives from typhoid fever and other diseases that can be prevented and treated.

For this reason, the United Nations Regional Information Centre (UNRIC) “asked” Myrtis to become a friend of the UN Millennium Development Goals and join, in her own unique way, the United Nations world campaign "We can End Poverty".

This is how Myrtis became a friend and supporter of the United Nations. She “assumed” her duties without delay by sending a message to world leaders who attended the UN Millennium Development Goals Summit of September 2010.

So, Myrtis is not any longer only “face to face with the past” but also “face to face with the future of humanity”.

 

MYRTIS, BINTI WA KIATHENA ALIYEISHI MIAKA 2500 ILIYOPITA, ANATUMA UJUMBE THABITI KWA ULIMWENGU.

 

myrtis_language_l

Jina langu ni Myrtis. Kusema kweli hili sio jina langu la asili. Nimefanya kupewa tu hili jina 'Myrtis' na wanaelimuchimbo walio ivumbua mifupa yangu kati ya miaka 1994-1995 kwenye kaburi la maiti ya watu wengi ambalo lilikuwa na mifupa ya maiti 150 huko Athens kwenye eneo la Kerameikos.

 Sura zangu zaonekana kama msichana wa karne ya ishirini na moja (21) lakini mimi naweza kuwathibitishia ya kwamba, mimi ni binti wa Kiathena mwenye umri wa miaka kumi na mmoja (11) aliyeishi na kufarikia Athens mnamo karne ya tano (5) BC.

Swali ni, yawezekanaje barubaru wa Kiathena wa enzi za kale kuja kuwa 'Rafiki wa 'Miaka Halufu' (Millennium Friend) wa Umoja wa Mataifa?

Wanasayansi wamethibitisha ya kwamba, nilikuwa mmoja ya wale watu waliofariki tokana na maradhi ya tauni yaliyowakumba wakaaji wa jiji la Athens wakati wa karne ya tano (5) BC. Pia wanajua ya kwamba kifo changu kilitokana na homa ya matumbo iliyoua mwanasiasa mwenye maarifa sana juu ya utawala mashuhuri Bw. Pericles pamoja zaidi ya thuluthi moja ya wakaaji wa jiji hilo. Wanasema pia, (wanasayansi) ya kwamba, tauni ndio iliosababisha wakaaji wa Athens kushindwa na Sparta kwenye vita vya Peloponese.

Fuvu la kicwa changu lilikuwa katika hali nzuri sana lilipopatikana, na hii ilimfanya mkufunzu mkuu wa Chuo Kikuu cha Madakitari wa Meno cha Athens (Athens University Orthodontics) Manolis J. Papagrigorakis kuingiwa na hamu ya kuitengeza sura yangu akisaidiwa na mtaalamu mwenzie. Sasa mwaona! Munaweza kuona matokeo yake kutoka hiyo picha yangu. Unaweza kuona juhudi ya kazi yao. Sura zangu karibu sana kufanana kama vile zilikuwa siku niliyofariki.

Mtaalamu Manolis J. Papagrigorakis alifikiria ya kwamba ufufuo wangu hautakuwa furusa tu ya kuonyesha ulimwengu sura za msichana aliyekuwa akicheza Acropolis wakati wenyeji wa Athens walipokuwa wakijenga Parthenon, la, alitaka 'marejeo' yangu yawe ni ujumbe thabiti kwa dunia na viongozi wake.

Kifo changu hakikuweza kuepukika. Katika karne ya tano (5) BC,  hatukuwa na ujuzi wala maarifa juu ya kutibu na kukinga maradhi yaliyoua watu.  Lakini ninyi, watu wa karne ya ishirini na moja (21), hamna sababu. Mko na kila aina ya ndia na rasilimali za kuokoa maisha ya mamilioni ya watu. Kuokoa maisha ya mamilioni ya watoto kama mimi ambao wanafariki tokana na maradhi yanayoweza kutibika na kuepukwa.

Miaka 2500 baada ya kifo changu, natarajia ya kwamba ujumbe wangu utawashughulisha na kuwapa moyo watu kufanya bidii hili 'Mikunjuo ya miaka helufu na Malengo yake' (Millennium Development Goals) kuhakikishwa.

Nisikizeni. Najua nisemalo. Msisahau kamwe ya kwamba mimi nina umri kuwashinda kwa hivyo nawashinda kwa hekima pia.

 

By:  Bi Maryam Tsertos, Yusuf (High school teacher)

 

 

Go to:

http://www.wecanendpoverty.eu/millennium-friends/millennium-friends.html

to see the original UNRIC page!

Επισκέπτες

  • Εμφανίσεις Περιεχομένου : 2925419

Η Μύρτις, φίλη του ΟΗΕ

Το μήνυμά της στους ηγέτες του κόσμου (μεταφράζεται σε 24 γλώσσες!)


Περισσότερα...